Jifunze maarifa mbalimbali ya kiroho na kimwili,tambua ulimwengu wa kiroho hasi na chanya,elimu zilizofichwa,zijue dawa na nguvu za asili za miujiza na utendaji wake. Call us +255 675 841177 email monicajonathan2000@gmail.com

Total Pageviews

Search

Friday, September 24, 2021

dawa hii ukiwa nayo unaingia popote bila kuonekana

SIKU MOJ NIKIWA KATIKA KIJIJI CHA NJUNGWA MKOANI MOROGORO,NIKIWA NA BABU YANGU MZEE CHILUNDA AKINIFUNDISHA BAADHI YA DAWA ZA MITI NA MAJINI NAKUMBUKA ALINIAMBIA HIVI ”BABU UNAONA HIZI KUNDE,UKIZIPANDA KWENYE JICHO LA PAKA ULIYEMCHINJA KWA MKONO WAKO NI DAWA MOJA KALI SANA INAYOWEZA KUKUFANYA UKAINGIA SEHEMU YEYOTE BILA KUONEKANA NA MACHO YA BINADAMU WA KAWAIDA”.ALINISHANGAZA SANA KWA KAULI HIYO NA NIKAWA NA SHAUKU KUBWA YA KUTAKA KUJUA SAYANSI HIYO YA AJABU KABISA,NDIPO ALIPOANZA KUNIFAFANULIA. INAVYOFANYWA
Kwanza kabisa apatikane paka mweusi ambaye hana kasoro yoyote yaani asiwe mlemavu wala kuchanganyikana na rangi nyingine katika manyoya yake mwilini. kisha zipatikane kunde(hizihizi za kula)takribani punje 10 kinachofuata ni kumchukua paka huyo na mhusika ambaye ndiye anayetaka kuitumia hiyo dawa anapaswa amchinje paka huyo kwa mkono wake kama anavyochinjwa kuku Baada ya kuhakikisha paka huyo ameshakata roho anachukuliwa na panachimbwa shimo sehemu iliyoandaliwa vizuri na anazikwa paka huyo hali ya kuwa macho yake yanatazama juu. Kwenye macho ya yule paka panawekwa udongo kidogo na kisha panapandwa mbegu tano kila jicho au hata zaidi,na panafukiwa vizuri pamoja na kuweka mbolea sasa hapo kazi anayoifanya mhusika ni kuhakikisha kila siku anamwagilia maji mpaka mimea ianze kuota kutoka kwenye mbegu hizo alizopanda ataendelea kuutunza kwa kiwango kikubwa kabisa mmea huo ulioota mpaka ukianza kuzaa kunde. Kunde zile zikishakomaa,anazichuma zote na sasa zile ndiyo hutumika rasmi kwa ajili ya kazi hiyo. Sasa endapo mtu huyu atataka aende sehemu na watu wa sehemu hiyo wasimuone(yaani anaweza akaja mpaka hapo ulipo akakaa pembeni yako anachungulia jinsi unavyosoma hii mada kwenye smartphone yako lakini wala humuoni wala kuhisi kitu)basi anakaa mbele ya kioo na anachukua punje moja moja anaweka mdomoni kisha anajiangalia kwenye kioo ikiwa atajiona kwenye kioo basi mbegu hiyo haifai anaweka pembeni anachukua nyingine ikiwa amachukua nyingine akaweka mdomoni na akaijitazama kwenye kioo hajioni hiyo ndiyo yenyewe anaihifadhi vizuri katika hizo kunde zote alizochuma anaweza pata punje 5-7 ambazo zitakuwa hazimuonyeshi kwenye kioo. sasa akitaka kwenda sehemu na asionekane anachukua ile mbegu anaweka mdomoni na kusema maneno fulani ya kikaguru kisha anatoka(hata kama umekaa nje ya mlango wake humuoni akitoka)anaenda alipokusudia na haonekani kweli. lakini haonekani na macho ya kawaida tu,mara nyingi wanapokutana na mtu mwenye majini makali njiani huweza kutokea shida kwani mtu yule huweza kumuona kwa uwezo wa jini na akamdhalilisha. Alipomaliza kuniambia hayo nilipigwa na butwaa na uso ambao dhahiri unaonyesha kutokuamini habari ile,naye aliliona hilo hatimaye akaniambia””sasa babu kama huamini ngoja nikuonyeshe kwa vitendo wewe kaa kimya” wakati huo mke wake(bibi)alikuwa ameshapika ugali na ameuweka pembeni akisubiri mchunga uliopo jikoni uive ili tujumuike kwenye msosi wa mchana. Alichokifanaya babu akachukua kikopo kweney mkoba wake wa uganga na akatoa humo ndani punje1 ya kunde kisha akatia mdomoni na kusema maneno fulani ghafla sikuweza kumuona na mara hiyohiyo nikamsikia bibi akilalamika ugali alioupika umechukuliwa hauoni!!! mara ghafla babu alitokea hapohapo akiwa sahani ya ugali mkononi huku akisema””nilikuwa nataka nimuhakikishie mjukuu wangu kuwa haya mambo yanawezekana”!