Wakfu hii inasaidia kama wewe ni kiongozi na unataka upendwe na watu wako,au upendwe kazini kwako na kupandishwa cheo,pia kama ni msanii na unahitaji kupata umaarufu inakufaa.
ukilivaa Talasimu hili a.k.a Wakfu utapendwa sana na watu,Unaliandika kisha unalifukiza kwa uvumba,udi na ubani maka na ubani mushatak kwa siku nzuri na saa nzuri haswa inapendeza siku ya ijumaa saa 1 asubuhi iwe ni mwanzo wa mwezi wa kiarabu.
ukisha kundika na kufukiza una mswalia mtume kwa idadi utakayoweza na kumuomba Mungu na ndani ya wakfu unaweka kidogo ambari safi na miski nyeupe ndipo unafunga hilo wakfu na kuzungushia kitambaa cheupe kwa nje na unajifunga mwiliniama kuweka kwenye walet
ni tarasimu ya uhakika na yenye kuleta majibu kwa haraka kwenye mambo hayo
