Jifunze maarifa mbalimbali ya kiroho na kimwili,tambua ulimwengu wa kiroho hasi na chanya,elimu zilizofichwa,zijue dawa na nguvu za asili za miujiza na utendaji wake. Call us +255 675 841177 email monicajonathan2000@gmail.com

Total Pageviews

Search

Friday, September 17, 2021

Je ni kweli kuna majini hutengenezwa na mwanadamu?

kuna baadhi ya watu wanaamini kwamba hapa ulimwenguni kuna majini ambao wameumbwa na mwenyezi mungu na kuna majini wengine wametengenezwa na sisi binadamu wenyewe. Jambo hili halina ukweli wowote ndani yake kwani majini pamoja na binadamu sote tumeumbwa na Mwenyezi mungu kwa lengo moja tuu la kufanya ibada na hakuna maandiko yoyote yaliyothibiti kwamba binadamu anao uwezo wa kutengeneza kiumbe cha Mwenyez Mungu. Ukweli wa jambo hili ni kwamba,kama nilivyosema hapo juu Binadamu hana uwezo ispokuwa Mwenyez mungu amemjaalia binadamu kuwa ni kiongozi wa viumbe vyote katika hali kama hii mwanadamu anao uwezo wa kumfanya kiumbe yoyote wa mwenyez mungu amtii na kumdhalilikia. mfano wa mambo haya ni kama vile Mbwa wa police ni wakali lakini wanatii kila amri ya polisi wao,au samaki aina ya pomboo[dolphin]wanavyotumika kutegua mabomu ya kivita baharini Hawa wote ni viumbe wa Mungu na wanamnyenyekea binadamu sio kwamba yeye ndiye amewatengeneza 'laa hasha''sifa ya uumbaji ni ya Mwenyez mungu tuu,kama kweli binadamu anaweza kumtengeneza jini sidhani km angeshindwa kumtengeneza binadamu mwenzie inawezekana huyo anayeambiwa anatengeneza majini hana hata mtoto mmoja na anamuhitaji kwanini asimtengeneze! Sasa kinachofanyika hapa ni kuwa binadamu yeyote atakayefundishwa utaalam maalum huwa anakuwa na uwezo wa kuwaita majini wabaya na wazuri pia kupitia utaalam huo na kuwatumia imma kwa mabaya au mazuri kwa kufanya nae mkataba maalum wa kazi ambao kila mmoja kati yao atapata maslahi yake....na hapa ndyo utaskia...oooh mzee fulani anatengeneza majini kumbe wala si kweli bali huwaita majini walewale ambao wapo na wameumbwa tayari na mungu aliyetuumba binadamu sote. mtu huyohuyo anayesemwa anatengeneza majini analala njaa kwa kukosa mboga basi si bora atengeneze nyama au samaki afanye apate kitoweo cha kulia ugali wake!!!!