NJIA YA UANGALIZI
Hii pia ni miongoni mwa njia wanazotumia wachawi hawa katika kumuita shetani wa kijini na kumtumia katika shugli zao za kiuchawi na kuwasababishia matatizo binadamu wenzao au hata wanyama mbalimbali wa kufugwa bila sababu yoyote ya msingi.
katika njia hii mchawi ambaye anataka kumuita jini huyu mbaya ni lazima avizie iwe usiku sana nyakati za giza, hutafuta sehemu nzuri ambayo ataweza kuziona nyota angani kisha hukaa hapo huku akiangalia nyota fulani na kuisubiri itokeze angani.(wenyewe wanaijua)
Ikishatokeza nyota hii huinuka mchawi huyu na huanza kuiomba kwa kusoma maneno maalum yenye code za kichawi.halafu anaanza kusoma tarasimu yenye maneno mazito ya kichawi na kuwaita majini waje kumtumikia,hakika maneno haya wanayoyasema ni mazito mno yasiyoweza kuandikika au kusemwa hadharani na mtu mwenye kumuogopa Mungu.
Baada ya hapo anafanya harakati fulani kwa kupeleka mikono yake juu na kuishusha chini[kama anavuta kitu]mwenyewe anadai anateremsha pepo wa nyota iyo lakini kwa hakika hii ni ibada anayoifanya kuiabudu nyota hii badala ya Mungu hata kama mchawi huyo alipofundishwa njia hiyo hakuambiwa hayo.
Basi kinachofuata hapo ni kuwa Mashetani yanaitikia amri ya mchawi huyu baada ya kuona na kupenda harakati zake anazozifanya kumkufuru Mungu na kuliongezea idadi jeshi la Ibilisi,na wanamfanyia kile kitu chake alichotia nia kukifanya huku yeye anaamini kuwa ile nyota ndiyo iliyomsaidia.
Nyota hii ambayo imesingiziwa uongo huu maskini huwa haijui kitu chochote kinachoendelea hapo bali ni maujanja tuu ya shetani katika kumzuga binadamu na kumtia dhambini.
Wachawi wenyewe wanaamini kuwa ukiwa umerogwa uchawi anaotumiwa jini wa namna hii,hauwezi kupona mpaka uaguliwe ndani ya siku ambayo nyota hiyo itaonekana tena na kuna nyota ambazo zenyewe kwa mwaka hutokea mara moja tuu,yaani uisubiri ile nyota tena na ikitokeza uiombe ikufungulie uchawi uliorogwa kwa kutumia jini wa njia hii.
