Jifunze maarifa mbalimbali ya kiroho na kimwili,tambua ulimwengu wa kiroho hasi na chanya,elimu zilizofichwa,zijue dawa na nguvu za asili za miujiza na utendaji wake. Call us +255 675 841177 email monicajonathan2000@gmail.com

Total Pageviews

Search

Sunday, October 3, 2021

Uhai,kifo,mwili na roho ni nini?

Uhai ninini? Uhai ni muunganiko wa mwili na roho... Hivi viwili kimoja kikiwa kinaonekana na kingine kikiwa hakionekani, ungano lao kwa usahihi wake ndio huleta kitu kinaitwa UHAI 2. Kifo ninini? Kifo ni hali ya kukoma kwa uhai... Kivipi? Roho inapojitenga na kile kiunganishi kingine kinachoitwa mwili ndio kifo hutokea... Kifo na mauti ni kitu kimoja na kile kile... 3.Mwili ninini? Mwili ni kibebeo, ni jumba ni kasha... Hapa ndio roho huja na kukaa ili kukamilisha tendo la uhai.. Na hivi viwili vikiwa pamoja ndio hutengeneza kitu kinaitwa nafsi au utambulisho... 4. Roho ninini? Roho ni nishati... Roho haionekani, haina umbo, haina sura, haina harufu... Hivyo vyote ni vya mwili... Lakini ili viweze kufanya kazi vinahitaji roho... Roho pamoja na kuwa ni nishati lakini katika na ndani ya mwili ni nishati yenye pumzi.. Hapa lazima tuelewane kuna nishati hazina pumzi Sasa tusonge mbele. Je kinachokufa ni mwili, ni (nafsi) au ni roho? Kwa tafsiri iliyozoeleka ya kibinadamu kinachokufa ni mwili.Kwa nini mwili? kwakuwa ndio kinachoonekana ndio visible,Ndio kilichoundwa ama kuumbwa.. Kila kilichoumbwa huwa na kikomo ama ukomo wa kuwa. Roho ni pumzi na ni nishati.Nishati wala pumzi havifi vilikuwepo vipo navitakuwepo milele. Lakini kwa usahihi kinachokufa ni NAFSI yaani utambulisho wako wewe.Na ndio maana tunaambiwa kila nafsi itaonja MAUT haisemwi mwili wala roho bali nafsi.. kwahiyo hata tunapofanya ibada na chochote kinachohusika na wafu tunadili na nafsi na sio mwili wala roho! Najua fika utasema mbona kuna roho mfu? Kiuhalisia hakuna roho mfu.. Ufu wa roho ni ile hali ya mwili kutengana na roho na hapo ndio tunapata tafsiri mbili moja ikiwa sahihi na nyingine ikiwa sio sahihi... Sahihi ni mwili mfu kwakuwa baada ya kutengana na roho wenyewe huendelea kuharibika kuoza na hatimaye kupotea milele Kinachobaki ni nafsi utambulisho ambayo haipo tena bali historia yake! Roho hubaki ikisubiri kiama ama kuingia kwenye utaratibu mwingine ama kugeuka mzimu......