Leo nataka tujifunze kitu na katika kitu muhimu ambacho unatakiwa kufundisha hata mwanao basi ni hiki cha leo maana kitamfanya asiishi kwenye giza
Leo nimewasogezea bi.dada huyu hapa anaitwa TIYE(Tye,Taia,Tiy,Tiyi) huyu ni BIBI yetu aliishi miaka ya 1338 BC na alikua ni mke wa farao AMENHOTEP III(wa tatu) na mtoto wao waliomzaa alikua Farao AKHENATEN hivyo yeye ndiye BIBI wa farao TUTANKAMUN
Yani huyu alikua ni Malkia(queen) mke wa farao AMENHOTEP na MAMA yake alikua akiitwa THUYU(Tyuju) BABA yake alikua akiitwa YUYA
Sasa tusimchambue sana huyu bibi kwakuwa babu zetu kwenye kuifadhi historia wapo vizuri tunaweza kufika mpaka kizazi cha 5 na tusimalize chimbuko lake yani babu zetu walikua hawana dogo kwenye kutunza historia walijua wajukuu zao ipo siku zitatufaa kama hivi leo
Sasa wakoloni na elimu yetu ya mchongo ya shuleni wanatuaminisha kuwa sisi tulikuwa tunaishi mapangoni na tulikua tunavaa mangozi ya wanyama kabla ya kuja wao yani wao ndo waliotuletea nguo na ustaarabu,sasa naomba tuangalie hio sanamu vizuri ya BIBI yetu malkia TIYE tuangalie kwa umakini sana katika yafuatayo.
ANGALIA HAIR STYLE YANI MTINDO NA UMARIDADI WA ALIVYOWEKA NYWELE
ANGALIA NA HILO VAZI. YANI NI GAUNI FLANI KALI SANA
sasa baada ya kuyaona hayo nakuachia kazi wewe mwenyewe jifikilie
mavazi walikuwa wanayatoa wapi
nani aliekua akiwapima na kuwashonea
nani alikua designer(mwanamitindo) wao
NOTE;Tupo tunafundishana kutumia akili kabla ya kuamini. Tupo hapa ili kuwatua mzigo wa ujinga uliowekwa na wakoloni katika kichwa chako. kupitia T'CHALLA na wakush wote tutaakikisha una FIKIRI kile unacho takiwa KUFIKIRI na sio KUFIKIRI kile wanachotaka UFIKILI
HOTEP HOTEP HOTEP
mwisho wa kumnukuu mkushi anayejulikana kwa jina la T'challa Sut'eh kutoka Dsm Tanzania
