Neno 'Astrology' limetokana na maneno mawili ya Kiyunani (Greek words) ambayo ni 'Astron' na 'Logos'
Astron means star,
sisi waswahili tunasema Nyota!
Logos means the Study of, yaani elimu ya . . .
Kwa hiyo Astron + Logos = Astrology (the study of stars)
Ndio maana tunasema ASTROLOGY ni ELIMU YA NYOTA au masomo yanayohusiana na Nyota.
Nyota (Star) kwa Kirumi huitwa 'Stella'
Stella ni nini basi kwa mujibu wa lugha kongwe ya Kikatini?
Ni viumbe vya kiroho vinavyokaa kwenye ulimwengu wa anga za mbali (cosmic realms)
Kwa mantiki hiyo Nyota ni viumbe hai, vinaishi kwenye anga za mbali!
Ninaposema anga za mbali ni pamoja na NJE YA DUNIA hii.
Kwenye elimu ya Anga (Astronomy) tunasoma kuhusu Nyota na Sayari (Star and Planets), vyote kama TERRESTRIAL OBJECTS, lakini kiuhalisia ni VIUMBE VYA KIROHO, vina uhai ingawa havina utashi, ni ROHO kwa lugha nyepesi zaidi.
Hizi roho (Nyota na Sayari) huathiri moja kwa moja maisha ya kila kitu kilichomo duniani ikiwa ni pamoja na maisha ya wanadamu wote, wanyama, mimea nk. kwa sababu ya muunganiko uliopo baina ya Celestial na terrestrial bodies.
Ndio maana watu wa zamani sana, walitumia Sayansi ya Nyota (Astrology) kutabiri mambo mbalimbali duniani kama vile majira fulani, matukio kadha wa kadha nk.
Kama ilivyo kawaida, kila majira yana namna ya kuifikia Sayansi fulani au Elimu fulani, hata watu wa kale, tofauti na sisi wa kizazi hiki, walikuwa na namna yao ya ku- study Nyota za angani na kutabiri mambo mbalimbali yajayo.
Matukio kama vita, njaa, zama za Wafalme fulani nk, vilitabiriwa kwa kutumia elimu ya Nyota.
Wataalam wa mambo ya Nyota huitwa Astrologers au Mamajusi.
Kiswahili cha kisasa wanaitwa Wanajimu!
ELIMU YA NYOTA ILIANZA LINI NA ILIANZIA WAPI?
Haijulikani waziwazi elimu hii ilianza lini, lakini inadaiwa ilianza karne nyingi sana kabla ya kuanzishwa kwa Taifa la Israel, Taifa maarufu na lenye historia ndefu sana duniani.
Maelfu ya miaka mingi kabla ya kuzaliwa Kristo Elimu hii ilikuwa maarufu sana Mashariki mwa Dunia na Nyanda za Kushi (Africa ya sasa)
Kwa hiyo Asili ya Elimu hii ni Mashariki mwa Dunia (Mesopotamian region) lakini wao waliichukua kutoka Kemet (Afrika) ambayo inadaiwa kuwa KITOVU cha elimu zote za kale!
Wafalme wakubwa sana walitabiriwa miaka mingi kabla ya kuzaliwa, kwa kuangalia Nyota!
Hii ina maana kwamba mtu kabla hajazaliwa anakuwa NYOTA (star) na anazaliwa ili awe Nyota inayong'aa zaidi (the Super Star)
Ndio maana kuna hili Neno 'Super Star' kwa watu wote wanaofanya vizuri sana kwenye fani, tasnia na taaluma mbalimbali duniani!
Hakuna mtu aliyezaliwa, isipokuwa kuwa super star.
Hii ya kuzaliwa na kuishi maisha ya ajabu ajabu (sub Star) ni kule kukosa utambuzi wa kimuunganiko baina ya mwili wa binadamu na yeye mwenyewe (nyota yake)
Dunia ina watu wema na wabaya.
Watu wabaya, wana uwezo wa kui- diverge nyota ya mtu ili isimfanye mtu huyo kuwa vile alivyopaswa kuwa.
Ndio maana kuna uchawi wa kuloga nyota, lakini pia na elimu ya kuunganisha nyota na muhusika wa hiyo Nyota ambayo baadhi ya Wataalam wa elimu hiyo huita kusafisha au kurejesha Nyota!
Kutokana na wingi wa watu wabaya duniani, ilifika mahali, baadhi ya dini zikazuia kabisa namna yoyote ya watu kujihusisha na Nyota kwa sababu mtu angefanikiwa 'kuchezea' Nyota yako angekuwa amefanikiwa 'kukumaliza' kabisa!
Vitabu mbalimbali vya kidini, vilipiga marufuku watu wasio waadilifu kujihusisha na mambo ya nyota kwa sababu elimu hiyo ilitumika zaidi kuharibu maisha ya watu, badala ya kustawisha, lakini haikuwa hivyo tangu mwanzo, bali ukengeufu, ukaidi na ubaya wa mioyo ya wanadamu ndio uliosababisha elimu hii adhimu kuonekana kama elimu ya uchawi/ uharibifu na wenye hekima wa kale wakatafuta namna ya kuizuia na kuificha!
Hata hivi leo, unaweza kutumia maarifa ya elimu ya Nyota kuharibu maisha ya watu (ukitaka) au kuyaboresha, kutegemeana na upande uliopo, kama ni ule wa uharibifu (gizani) au ule mwingine wa nuruni!
Uchaguzi ni wako, unataka kufahamu elimu hii ya Nyota kwa maslahi gani.
Kwenye masomo haya ya Nyota, tunasema NYOTA NI WEWE na WEWE NI NYOTA!
Ilivyo Nyota yako ndivyo utakavyokuwa na wewe, isipokuwa mtu mwovu aamue kuchezea nyota yako!
kama unahitaji ushauri kuhusu masuala ya kinyota,kuunganisha nyota,kusafisha ,kurejesha n.k wasiliana nasi.
email.
monicajonathan2000@gmail.com
