Jifunze maarifa mbalimbali ya kiroho na kimwili,tambua ulimwengu wa kiroho hasi na chanya,elimu zilizofichwa,zijue dawa na nguvu za asili za miujiza na utendaji wake. Call us +255 675 841177 email monicajonathan2000@gmail.com

Total Pageviews

Search

Sunday, October 3, 2021

Mmea wa Dieffenbachia wenye jina maarufu la dumb cane ni mmea hatari wenye sumu

Wengi tunapanda majumbani mmea huu kama maua yanayopendeza hivyo ni muhimu kuujua vizuri mmea huu wenye sumu hatari inayoweza kuuwa
Mmea wa dieffenbachia ujulikanao kama dumb cane ni genus ya mmea wa tropiki wa familia ya Araceae. Mmea huu asilia yake umetoka Mexico na Argentina ya kusini. Chembe hai za dieffenbachia( dumb cane) zina mdungo mkali wa kemikali ya sumu iitwayo calcium oxalate crystals ziitwazo raphides. Raphides ikiingia kwenye mwili wa binadamu huleta mwasho na kusababisha mwili wa binadamu kuvimba nà hatimaye kusababisha kifo. hautakiwi kuwa karibu na watoto wadogo ama wanyama kama mbwa ama paka na wengineo